Kisa Changu Podcast: Nina hisia tofauti kimwili; si tatizo la kiakili
Published Jun. 25, 2022
00:00
00:00

Elidah Maita mkazi wa Roysambu, Nairobi ni mwanaharakati wa kutetea haki za watu walio katika uhusiano wa jinsia moja na wa jinsia tambuka yaani ''Queer''. Anasema alianza kuhisi akiwa tofauti na wasichana wengine akiwa na umri wa miaka kumi pekee na licha ya kumuuliza mamake mzazi maswali chungu nzima hakupata maelezo ambayo yangemsaidia kuelewa hali yake. Maita mwenye umri wa miaka 25 anasema ari yake ya uanaharakati na kuihamasisha jamii kuhusu ''LGBT-Q+'' ilitokana na changamoto alizopitia alipokuwa mdogo. Maita anasema watu kama yeye mbali na unyanyapaa wengine wamedhulumiwa bila sababu hali inayowasababishia wengine kukumbwa na msongo wa mawazo huku wengine wakijiua. Mfano anasema mienendo yake na hata jinsi anavyovaa huwafanya baadhi ya watu kumtenga. Hata hivyo, anasisitiza hilo halitazima juhudi zake za kuieleimisha jamii kuhusu LGBT-Q+. Fahamu mengi zaidi kumhusu Maita katika makala ya ''Kisa Changu Podcast'' na Robert Menza.