Kisa Changu Podcast: Nabaguliwa kwa kuwa nina ulemavu wa ngozi 'albinism'
Published Jun. 18, 2022
00:00
00:00

Denis Kazungu ni mwenye ulemavu wa ngozi yaani albinism. Kazungu mwenye umri wa miaka 29 na ambaye ni mkazi wa Malindi-Airport, Kilifi anasema hali yake imemsababishia changamoto nyingi tangu alipozaliwa hadi sasa. Kazungu amepitia unyanyapaa; amebaguliwa si tu na jamii bali pia kwenye maeneo ya kazi akisema ulemavu wake umesababisha kampuni nyingi kutilia shaka uwezo wake wa kutekeleza majukumu. Je, amefanikiwa vipi na hata kupiga hatua maishani licha ya changamoto hizo? Sikiliza masimulizi yake katika makala yafuatayo ya ''Kisa Changu Podcast'' na Robert Menza.