Kisa Changu Podcast: John Kiriamiti - maisha ya uhalifu; alianzia uandishi jela
Published Feb. 03, 2022
00:00
00:00

Anafahamika kufuatia visa vyake vya wizi sugu wa pesa katika benki wakati wa miaka ya 70. John Kiriamiti aliacha masomo akiwa katika kidato cha kwanza akiwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Prince of Wales ambayo sasa ni Nairobi School, na hapo ndipo alipoanza uhalifu. Hata hivyo, wasemao husema kwamba siku za mwizi ni arubaini. Kiriamiti pamoja na wenzake walikamatwa na kuhukumiwa jela kutokana na uhalifu huo. Akiwa jela, John Kiriamiti alianza uandishi wa vitabu, ambavyo baadaye vilikuwa maarufu nchini na kupendwa sana hasa na wanafunzi. Vitabu vilivyoandikwa na Kiriamiti ni kama My Life in Crime, My Life With a Criminal, My Life in Prison. Fahamu zaidi kuhusu maisha yake katika masimulizi yafuatayo.