Watu sita wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa baada ya matatu iliyokuwa ikitoka mjini Eldoret kupoteza mwelekeo na kubiringirika kwenye eneo hatari la Sachangwan Barabara Kuu ya Nakuru-Eldoret.
Kamanda wa Polisi wa Molo Mwenda Muthamia, amesema kuwa wanawake wanne na mwanamume mmoja wamefariki dunia papo hapo huku abiria wengine wanane wakijeruhiwa jana usiku. Majeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Molo