×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Mfanyabiashara, Jimi Wanjigi aachiliwa huru kufuatia agizo la mahakama

News

Mfanyabiashara, Jimi Wanjigi ameachiliwa huru baada ya kukesha katika seli za Kituo cha Polisi cha Kamkunji kufuatia kukamatwa kwake siku ya Jumanne katika ofisi zake za Kwacha eneo la Westlands jijini Nairobi.

Wanjigi ameachiliwa kufuatia agizo la Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani, Bernard Ochoi baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kwamba kulikuwa na agizo lililotolewa jana la kuzuia kukamatwa kwake. Afisa wa mashtaka, Eveline Onuga amesema kwamba amezidurusu stakabadhi za agizo la kutokamatwa kwa Wanjigi na kubaini zilikuwa halali.

Ochoi aliafikia uamuzi huo baada ya kusitisha kikao cha kesi dhidi ya Wanjigi kwa takriban saa moja ili kushughulikia malalamishi yaliyowasilishwa na wakili wake, Willis Otieno kwamba mteja wake alikuwa amekamatwa kinyume na sheria. Hakimu huyo vilevile amedumisha agizo la kutokamatwa kwa mkewe Wanjigi, Irene Nzisa japo amesema washtakiwa wengine sita wanastahili kukamatwa na kuwasilishwa mahakamani siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Alipowasilishwa mahakamani leo asubuhi, upande wa mashtaka ulipendekeza mashtaka sita dhidi yake pamoja na watu wengine saba ambao hawakuwa mahakamani. Mashtaka hayo ni kughushi ramani ya  kipande kimoja cha ardhi chini ya jina Dodhia Foam Limited kati ya tarehe 9 Aprili mwaka 2010 na Juni tano mwaka 2018.

Shtaka la pili ni kuhusu kughushi stakabadhi za umiliki wa ardhi io hiyo na kuwasilisha cheti kilichodaiwa kutiwa saini na Kamishna wa Ardhi, Wilson Gachanja.

Shtaka jingine ni dhidi yake na mkewe Irene Nzisa vilevile John Nyanjua Njenga ambapo wameshtakiwa kwamba  mnamo Mei 30 mwaka 2018 waliwasilisha stakabadhi ghushi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kudai kubadili jina la kipande cha ardhi kilichokuwa chini ya jina la Dodhia Foam hadi Auream Limited. 

Vilevile Wanjigi na washtakiwa wenza wanakabiliwa na tuhumza kupanga kuilaghai shilingi milioni hamsini na sita Kampuni ya Kenroid kwa misingi kwamba walikuwa na uwezo wa kuiuzia ardhi.

Akizungumza baada ya kuachiliwa  huru, Wanjigi amesema ilikuwa mara yake ya kwanza kulala katika seli za polisi huku akiwashtumu waliochangia kukamatwa kwake kinyume na maagizo ya mahakama.

Aidha amesema kwamba atawashtaki maafisa waliomharibia mali yake wakati walipozimamia ofizi zake jana. Amesema kwamba atatathmini kiwango cha uharibifu ambao unakisiwa kuwa wa milioni kumi kabla ya kuwasilisha mashtaka.

 

 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week