×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Chebukati apinga kupotea kwa vifaa vya Kiems kits

News

Tume ya uchaguzi, IEBC imepuuza madai ya kupotea kwa vifaa vya kielektroniki vya Kiems kits elfu tatu na kusema uvumi huo ni propaganda.

Kupitia taarifa, Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati badala yake amefafanua ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuwa kuna vifaa vya uchaguzi vikiwamo BVR vya kuwasajili wapiga kura, Kiems kits na vipakatalishi ambayo vimepotea.

Chebukati amebainisha kuwa vifaa vilivyoptea ni BVR wala si vile vya Kiems kits ambayo anasema vilinunuliwa mwaka wa 2012 na muda wake wa matumizi umekamilika wala havijatoweka.

Taarifa yake imejiri miezi mitatu baada ya ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali  Nancy Gathungu kufichua kupotea kwa BVR 3,925, Kiems kits 7 na vipakatalishi 392 miongoni mwa vifaa vingine vya uchaguzi.

Hata hivyo, Chebukati amesema kuwa vifaa vyote vya Kiems kits viko tayari kusambazwa kwa maafisa watakaosimamia uchaguzi pamoja na mashine za kuweka umeme, power banks mbili kwa kila kifaa endapo umeme utapotea.

Related Topics