×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Safaricom yazindua kampeni ya ''Tuinuane''

Living

Kampuni ya Safaricom imezindua kampeni mpya kwa jina ''Tuinuane'' inayolenga kuwapa Wakenya moyo wa kusaidiana.Chini ya Kampeni hiyo Safaricom inalenga kuiwezesha jamii kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata vifaa vya masomo kwa haraka kando na kuzindua huduma mpyana za kisasa kwa manufaa ya wateja wake.Afisa Mkuu Mtendani wa Safaricom Peter Ndegwa amesema kampeni ya ''Tuinuane'' imetokana na moyo wa Wakenya wote wa kujitolea kutoa usaidizi.

Chini ya Mpango huo, Wakfu wa Safaricom kupitia mpango wa Ndoto Zetu itaimarisha ushirikiano wake na jamii.

Tangu kuanzishwa kwa Ndoto Zetu mwaka 2019 zaidi ya Wakenya milioni 3 wamenufaika, huku mwaka huu Safaricom ikilenga kuwafikia Watu milioni mbili zaidi kupitia miradi mbalimbali itakayogharimu shilingi milioni 100.Mkenya yoyote anayehisi kwamba angependa kuisaidia jamii yake anaweza kutuma ombi kupitia wavuti wa Safaricom https://www.safaricomfoundation.org/ndotozetu/ au kuyatembela maduka ya Safaricom kote nchini na kujaza fomu ili kuiweka jamii yake katika nafasi nzuri ya kunufaaika.Katika elimu Safaricom imeshirikiana na washikadau mbalimbali ili kuhakikisha kunakuwapo na vifaa vyenye gharama ya chini vya masomo. Miongoni mwa washikadau hao ni Shupavu 291 inayoweza kupatikana kupitia ujumbe mfupi kwa shilingi 4 tu kwa sku au wavuti wa elimu wa Safaricom unaoweza kufikiwa kutumia data ya 200mbs kwa shilingi 20 pekee.Safaricom imanzisha mpango wa kutoa bandali za interneti yaani bundles za Tuinuane zitakazowawezha watea wake kupata ofa za interneti dakika za kuia simu na kutuma ujumbe mfupi kwa shilingi ishirini pekee.

Mpango wenyewe unajumuisha 1GB ya data inaytumika kwa saa moja dakika za mzungumzo ya simu kwa saa nzima na wamasiliano kupitia ujumb mfupi kwa siku moja. Ili kupata ofa hizi mteja anastahili kubonyeza *444*22#.Safaricom pia imewahsuri wateja wake kutumia Bonga Points kujiinua ahu kuwainua wenzao.

Wakati huo huo, katika wikina miezi michache ijayo kampuni hiyo inalenga kuzindua mipango kadha akupitia kampeni hiyo ya Tuinuane ukiwamo uzinduzi wa akaunti ya wateja walio na kati ya umri wa miaka 10 na 18 na kuanzisha mpango wa kuwekeza ambapo wateja wa M-pesa watapata fursa ya kuwekeza na kupata faida.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles