×
App Icon
The Standard e-Paper
Home To Bold Columnists
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: corporate@standardmedia.co.ke

Huenda kalenda ya masomo ikavurugika

Licha ya serikali kutangaza kwamba shule zinatarajiwa kufunguliwa Alhamisi wiki ijayo, uwezekano wa ratiba ya muhula huu kuvurugika unaendelea kuongezeka. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Elimu, Prof George Magoha, likizo iliyoanza jana inafaa kukamilika Jumatano wiki ijayo kwa imani kwamba shughuli katika shule ambazo zinatumika katika vituo zitakuwa zimekamilika.

Hata hivyo uhalisia kutokana na historia ya uchaguzi wa mwaka 2017 uliofanyika tarehe 8 Agosti, matokeo yalitangazwa tarehe 11 yaani siku tatu baadaye kumaanisha huenda matokeo ya mwaka huu yakatangazwa tarehe 12 ama kuchelewa hata zaidi.

Hali hii huenda ikawaweka wazazi ambao wanao wanasoma mbali na nyumbani katika suintafahamu ya kuwaacha wanao wasafiri pasi na ufahamu wa jinsi matokeo yakakavyopelekewa. Kadhalika, kuna uwezekano mkubwa wa matokeo hayo kupingwa mahakamani ama kurejelewa.

Akizungumza wikendi, Waziri Magoha alikuwa amewatahadharisha wazazi kutarajia lolote iwapo mabadiliko yatahitajika katika ratiba.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles