×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Kenya Kwanza yasisitiza mkutano wake wa mwisho utafanyika Nyayo

Living

Katibu Mkuu wa Chama cha UDA, Veronica Maina amesisitiza kwamba Kenya Kwanza itafanya mkutano wake tarehe 6 Agosti katika Uwanja wa Michezo wa Nyayo, akipinga kupokonywa leseni ya kuendesha mkutano siku hiyo. Kwa mujibu wa Maina, tayari Kenya Kwanza imelipia uwanja huo na hawatakubali kubatilishwa.

Ijumaa wiki hii Kamati ya Kampeni za Ruto iliwasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya Idara ya Michezo kusema kwamba uwanja huo utatumika kwa mikutano ya amani.

Hayo yanajiri huku Muungano huku muungano huo ukiwateua Brian Mbugua na Anthony Mwaura kuelekea Ugiriki kushuhudia uchapishaji wa karatasi za kupigia kura.

Katibu Mkuu wa Chama cha UDA, Veronica Maina amesema wawili hao wataondoka nchini leo usiku(Jumamosi).

Akihutubu katika kampeni za kumpigia debe mgombea urais wa UDA, William Ruto, Maina aidha ametaka Tume ya Uchaguzi IEBC kuendesha uchaguzi huru na wa haki, akiwahimiza Wakenya kudumisha amani.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles