×
App Icon
The Standard e-Paper
Join Thousands of Readers
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Mabalozi wahimiza kuandaliwa kwa uchaguzi wa amani

Living

Na, Beatrice Maganga Mabalozi wahimiza kuandaliwa kwa uchaguzi wa amani Mabalozi wa mataifa ya kigeni wanaohudumu humu nchini wametoa wito wa kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu huru na wa haki humu nchini. Wajumbe hao wametoa wito huo wakati walipofanya kikao na Kaimu Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi, Fred Matiang'i.  Akiwahutubia wanahabari baada ya kikao hicho, Matiang'i amesema miongoni mwa yaliojadiliwa katika kikao hicho ni kuhusu namna maafisa wa usalama wanashirikiana na Tume ya Uchaguzi, IEBC ili kufanikisha uchaguzi mkuu huru na wa haki. Matiang'i  amesema ni jukumu la IEBC kuandaa uchaguzi huku maafisa wa usalama wakihusishwa katika kuipa usaidizi IEBC kutekeleza jukumu lake la kikatiba. Wajumbe hao wametoa wito kwa serikali kuipa tume hiyo raslimali za kutosha ili kufanikisha maandalizi ya uchaguzi. Kikao hicho kimejiri wakati ambapo baadhi ya mataifa yametoa ilani kwa raia wake wanaoishi humu nchini kuwa waangalifu wakati huu wa uchaguzi. Mataifa ya Uingereza  na Urusi ni miongoni mwa yale ambayo tayari yametoa ilani kwa raia wake.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles