×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Gavana Gachagua ajitetea vikali

Living

Na, Mike Nyagwoka

Gavana wa Nyeri, Nderitu Gachagua amekana tuhuma zote zinazomkabili kwenye hoja ya kumbandua iliyowasilishwa katika Seneti. Akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha Seneti kujadili hoja dhidi yake, amesema tuhuma za ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya mamlaka zimechangiwa na mivutano ya ubabe baina yake na wapinzani wake.

Kwenye kikao cha Jumanne, Seneti imeorodhesha tuhuma nne zilizowasilishwa na bunge la Kaunti ya Nyeri zikiwamo za kukiuka sheria za ununuzi na utumiaji mbaya wa fedha za kaunti. Aidha, kwa mujibu wa tuhuma hizo, Gachagua alitumia kiasi cha fedha kilichozidi kilichotengwa na Mkuu wa Bajeti.

Serikali ya Kaunti kupitia wakili, George Ng'ang'a vilevile imepata fursa ya kuwasilisha hoja dhidi ya gavana huyo huku ikimshtumu kwa kutowajibikia miswada mbalimbali ambayo huwasilishwa mbele yake mbali na kutohakikisha wafanyazi wa kaunti wanalipwa mishahara yao kwa wakati.

Vikao hivyo vitaendelea Jumatano ambapo Gachagua atapata muda wa kutosha kujibu madai yaliyoibuliwa dhidi yake huku vikao vya mwisho vikiandaliwa Alhamisi. Baada ya vikao vya Alhamisi, bunge hilo litapiga kura kwa kila tuhuma kabla ya kutoa uamuzi wake wa mwisho. Bunge la Kaunti ya Nyeri liliidhinisha hoja ya kumwondoa ofisini takribani wiki tatu zilizopita.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles