Na,Hassan Ali
Tuanze kwa kuangazia ratiba ya mashindano ya olimpiki huko Rio Brazil ambayo yanatarajiwa kufunga milango yake rasmi mnamo Jumapili. Kenya ingali na matumaini ya kutwaa medali zaidi katika mashindano ya kutembea kilometa 20 leo usiku saa tatu unusu. Baadaye alfajiri zikiwa zimesalia dakika 20 kugota saa kumi na moja, kutaandaliwa fainali ya mbio za mita alfu tano wanawake, timu ya Kenya ikiongozwa na mshindi wa fedha majuzi mbio za mita alfu kumi Vivian Cheruiyot. Hapo kesho saa kumi kasoro dakika tano Wakenya watashuhudia fainali ya kurusha mkuki tukiwa nyuma ya bingwa wa mshindano ya Afrika na Jumuiya ya Madola Julius Yego. Kiziba mkonga kitakuwa Jumapili saa kumi unusu mchana mbio za marathon wanaume. Tayari Kenya imetwaa dhahabu kwenye marathon kina dada kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii. Kila la kheri Team Kenya
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.