×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Ahmed Darwesh: Wasichana wa leo hawawezi hata kuchemsha mayai

Living

Leo ningependa kuwaandikia wanandoa na wapenzi walioko kwenye uhusiano kwa muda mrefu.

Wengi wameshindwa kuzidhibiti ndoa zao na hata uhusiano wao kutokana na kuwa na mapenzi chapwa! yasiyokuwa na uhai.

Mapenzi yanahitaji ufundi, tena ufundi wa hali ya juu. Kuanzia kwenye mambo ya ndoa yenyewe, usafi wa nyumba na hata mapishi kwa ujumla. Wajuzi wa mambo wanasema njia moja ya pekee ya kuuteka moyo wa mwanamume ni kupitia tumbo lake.

Lakini ushawahi kujiuliza, je wasichana wa karne hii ya utandawazi wanajua kupika au huishilia tu kula vyakula matabwatabwa ambavyo haviliki wala haviangaliliki.

Wasichana wengi tunaoishi nao katika jamii ya kileo hawafai hata peni. Labda ni kutokana na mazingira wanayoishi au uvivu wa kisasa umewatawala kiasi ya kwamba hawajui hata kupika chai ya rangi, wala kuchemsha mayai, kwa kuwa kila kitu wanafanyiwa na wafanyikazi wa nyumbani.

Natija ya yote haya huwa ni kukatizwa ghafla kwa ndoa au hata kuwachwa na waume zao wasijue wataanzia wapi baada ya kupika mashendea na kumlisha mume vibanzi na kuku wa kukaanga kutoka mikahawa inayofahamika ya hapa jijini.

Wachache wao wakijua kupika maharage, basi itakuwa ni maharage wee hadi kiama. Kwanini basi mume asisinywe na kula chakula kimoja kila siku. Si aibu kusema kuwa haujui kupika kwani muda wa kujirekebisha na kujifunza bado unao, nakushauri tu uulize kwa wenzi, rudi ngumbaro ya unyumba ili ujifunze namna ya kupika vyakula vya tunu.

Vyakula vinayojulikana kama fast foods, kama vile Burgers, Chips na Chicken na vyakula vyengine vya ajabu ajabu havitakusaidia katika kudumisha ndoa yako, bali vitaivunja kabisa.

Mwanamume anahitaji malezi na yakikosekana huwa ni sawa na shamba bila ya palizi. Mume muenge enge kwa mapishi na kumpa kitu roho inataka. Asitake maini ukampa kabeji, utakuwa umemsaliti.Chakula cha kumfurahisha mume ni kile kilichopikwa kwa manjonjo na kutiwa nakshi ya viungo vya kupendeza kupitia ubunifu wa hali ya juu. Kuwa mbunifu, jikoni, sebuleni na hata kitandani hapo utainusuru ndoa yako. Mupo?

Yakikugusa wasiliana nami kupitia [email protected] ama the [email protected]

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles