Ngoma ikilia sana hupasuka na tamu ikizidi sana huchachuka na hata kuwa chungu kama shubiri. Hapa twamzunguzia rais jirani wa Tanzania John Pombe Magufuli ama kama Wabongo wanavyomita ‘Uncle Magu’ ama ‘JPM’. Bwana huyu alikuja kwa vishindo vikuu vya kuleta mabadiliko makuu Tanzania.Aliwashtua wengi kwa kupigana kwa jino na kucha dhidi ya zimwi la u?sadi. Tofauti na mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete alopenda anasa za kutembea kama mtalii duniani ‘uncle Magu ‘ hana upuuzi huo kwani hakupenda starehe za kitalii za kupanda ndege.
Tukimgusia Kikwete ni kuwa alikuwa kiongozi aliyependa sifa na kujirembesha kwa masuti makubwa makubwa Kikwete alikuwa kama msanii alijirembesha kitanashati na kunyowa kama kijana wa kizazi kipya huku akitabasamu ovyo ovyo kama bwana harusi. Bwana msa? huyu alikuwa daima na masafari yasoisha ya kile alichoita safari za kuleta maendeleo na mfano wa Tanania.