Michemko ya siasa za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta inazidi kushika kasi katika eneo la Bonde la Ufa nyumbani kwa Naibu wa Rais Dkt. William Ruto baada ya Seneta wa Baringo, aliyepia mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi, kuvikwa taji la kitamaduni na kutawazwa kuwa mzee wa jamii ya Wakalenjin. Kwenye ha? a iliyofanyika siku ya Jumamosi katika eneo la Mlima Elgon, Mwana wa Rais Mstaafu Daniel arap Moi, Gideon Moi alisimikwa kuwa mzee wa jamii ya Kalenjin.
Ni katika sherehe ambayo hufanyika baada ya mashauri na maelekezo kutoka kwa wazee wa Kikalenjin. Ha?a ya usimikaji hufanyika tu pale ambapo wazee wa jamii wanapopata ufunuo maalum na hupewa kiongozi aliye na nyota na ari ya kuongoza jamii kwa ujumla na wala sio jamii yake ndogo ama ukoo anakotokea kuamua. Eneo la Mlima Elgon linaaminika kuwa ndilo chimbuko la Jamii ya Wakalenjin kihistoria kwani inasadikika kwamba jamii hiyo iliingia Kenya kupitia mlima huo ulioko kaskazini Magharibi mwa nchi. Jamii ya wakalenjin pia inaamini kuwa sauti ya mababu zao imesalia katika mlima huo na kila jambo linalohusu uongozi wa nchi lazima litokee katika mlima huo kabla ya kutangazwa ama kupokelewa kwingineko zinakopatikana kabila tisa za jamii ya Wakalenjin.