Kiongozi wa wachache katika bunge la Seneti James Orengo na kiongozi wa ODM Raila Odinga katika mkutano wa siasa ya zamani. [Picha: Standard]
Ama kwa kweli mambo yanayoendelea ndani ya nyumba za watu unaweza kupigwa na butwaa kusikia haswa nini kinachoendelea kila kukicha. Baadhi ya viongozi wa chama maarufu cha ODM ambao daima wamemkiria kinara wake wa kitaifa Raila Odinga “Baba” kuwa kuwa ni simba aliyenyeshewa na mvua baada ya mkono wake wa buheri na Rais Uhuru Kenyatta, walipigwa na mshangao wakati alipowakemea miongoni mwa viongozi wake ambao huropokwa maneno bila kupima uzito wake.