Mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio imekosa kuelewana kuhusu kujumuishwa kwa Mbunge wa Eldas Aden Keynan kwenye kamati ya mazangumzo yasiyokuwa na miegemeo Bipartisan kuhusu masuala yaliyoibuliwa na Azimio.
Aidha licha ya kutoafikiana kuhusu suala hilo, mirengo hiyo miwili imeafikiana kwamba mazungumzo hayo yaendelee wakati ambapo suala hilo linashughulikiwa na viongozi wa mirengo hiyo Rais William Ruto na Raila Odinga.