Maajabu ya kuku kuangua kifaranga cha miguu minne Kakamega

Wenyeji wa kijiji cha Emasera wadi ya Butsotso mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wamebaki vinywa wazi baada ya kuku kumangua kifaranga mwenye miguu minne.

Kulingana na taarifa zilizofi kia meza ya Pambazuko ni kuwa kifaranga huyo mwenye afya nzuri na maumbile ya kushangaza alianguliwa wa kwanza, siku 5 kabla mayai  mengine yaliyo lalishwa na kuku huyo kuanguliwa kisa ambacho kilishangaza na kuwavutia wenyeji kushuhudia malimwengu hayo.

Hellen Muranditsi  ni mama mwenye kuku huyo na anasema hajawai ona kisa kama hicho huku akidai tangia kuaguliwa kwa kifaranga huyo siku tano zilizopita mayai   mengine bado hayajaanguliwa akihusisha kisa hicho na baraka kwa familia hiyo.  

Hii ni baraka kwetu, tangia kuaguliwa kwake hakuna mayai ingine imeaguliwa hii ikiwa siku ya tano tangia kuaguliwa kwa kifaranga hiki,” Akasema Hellen.

Ni tukio lililowavutia wenyeji wa eneo hilo ambao walimiminika kwa boma hilo kushuhudia kisa hicho wengine wakiwatahadharisha jamaa wa boma hiyo na tukio hilo kama dalili ya mkasa kutokea kwani kisa hicho si cha kawaida.

“Huwa naskia ng’ombe amezaliwa na midomo miwili, leo nimeshudia kuku wa miguu minne, kisa hiki si cha kawaida na huenda nikuwaonya jamaa wa boma hili dhidi ya mikasa ya baadaye,” Akasema mmoja wa wakaazi.

Haya yanajiri huku kisa kingine cha kustaajabisha kikitokea kaunti hiyo hiyo   ambapo jamaa mmoja aliandaa hafl a ya mazishi ya kuku wake aliyeaga akiwa analalia mayai.

Joseph Omulai mwanaume kutoka kijiji cha majimazuri eneo bunge la Lugari kaunti ya Kakamega anasema alihuzunishwa na kifo cha kuku wake aliyeaga baada ya kupigwa na mtu asiyejulikana alipokuwa ameenda kutafuta riziki yake ya kila siku huku akisema alistahili kufanyiwa mazishi ya heshima.

“Baada ya kumpea chakula na kuondoka nilirudi jioni nikajaribu kumrushia chakula lakini hakuonekana kushughulika nilimkaribia na nikapata ameaga, ni huzuni kwangu,” Akasema Omulai.

Kama tu ile ya binadamu omulai  aliimba nyimbo za kuomboleza na kusoma biblia kabla ya kuufunga mzoga huo kwenye shuka nyeupe na baadaye kumzika kisha kulifunika kaburi lake kwa saruji huku pia akipanga kumfanyia kumbukumbu.  

Alizika kuku, maya pamoja na sufuria iliyokuwa imelaliwa, kulikuwa hata na disko matanga,” Akasema jirani wake.

Ni kisa kilichowashangaza wenyeji wa eneo hilo.

“Nimeshangazwa na kitendo hiki, sijawai skia mtu anazika kuku kwa kumfanyia ibada, ni kichekesho pia ni huzuni,” Akasema mmoja wa wakaazi.

Kilichosalia ni kusubiri kuona kama hafl a ya makumbusho itafanywa? Na ni nani wataalikwa huku eneo hilo likiwa Magharibi mwa Kenya tunatarajia kuona kama waalikwa watachinjiwa kuku.

Related Topics

Kakamega Chicken