Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga, imetoa wito kwa Wakazi wa Kaunti za Mombasa, Kilifi, Lamu, Kwale na Tana River kuwa makini kwani mvua kubwa inatarajiwa kunyesha maeneo hayo kuanzia leo.
Mvua hiyo kubwa yenye waviwango vya milimita 20, inatarajiwa kushuhudiwa leo huku viwango hivyo vikiongezeka hadi milimita 40 kufikia tarehe saba. Aidha itapungua tarehe nane huku ikiambatana na upepo mkali.