Mwalimu Samuel Murithi azindua filamu na muziki kwa watu wasiokuwa na uwezo wa kusikia kwa mara ya kwanza

Kwa mara ya kwanza nchini, mwalimu mmoja kwa jina Samuel Murithi amezindua filamu na muziki kwa watu wasiokuwa na uwezo wa kusikia.

Muriithi ambaye alipoteza uwezo wa kusikia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita , amesema watu wasiokuwa na uwezo huo hutatizika katika kuelewa miziki na filamu kwani hakuna utafsiri wowote.

Amesema uzinduzi wake utawapa fursa watu hao katika kushiriki kwenye filamu vilevile nyimbo kama watu wengine wenye uwezo wa kusikia.

Muriithi amedokeza kwamba uzinduzi wake ulichochewa na wanafunzi wanaoshiriki tamasha ya muziki nchini. Tayari amezindua albamu ya kwanza kwa watu wasiokuwa na uwezo wa kusikia.