Wanafunzi wawili ni miongoni mwa washukiwa watatu wa ulanguzi wa dawa za kuelvya

Wanafunzi wawili ni miongoni mwa washukiwa watatu wa ulanguzi wa dawa za kuelvya ambao wamekamatwa. Wawili hao Chris Odhiambo, mwenye umri wa miaka ishirini na miwili na Raymond Mwilo mwenye umri wa miaka ishirini ,walikamatwa wakiwa wanaelekea hapa jijini Nairobi.

Kulingana na Idara ya Upelelezi DCI walikuwa wamejifungia dawa hizo kwenye migongo ili wasipatikane na polisi. Watendelea kuzuiliwa hadi kesho watakapofikishw amahakamani.

Wakati uo huo, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Mombasa Johnston Ipara amewaonya watu ambao wanaendeleza ulanguzi wa mihadarati kwenye maeneo ya jiji hilo kwamba watakabiliwa kwa mjibu wa sheria.

Amesisitiza kwamba idara ya Polisi inaendeleza msako wa kuwatia nguvuni walanguzi hao sawa na wale ambao wamekuwa wakitumiwa kusafirisha mihadarati ndani na nje ya Mombasa.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya maafisa wa polisi mjini Mombasa kumtia mbarini mlanguzi sugu wa mihadarati akiwa na kilo moja ya dawa hizo aina ya Heroin.

Takwimu ya Mamlaka ya Kudhibiti  Unywjai Pombe na utumizi wa dawa za kulevya NACADA zikionesha kwamba jumla ya watu 24, 500 kwenye Kaunti ya Mombasa wameathiriwa na mihadarati.

Related Topics