ICC yathibitisha kupokea ombi la kutakiwa kuwachunguza viongozi wa Muungano wa NASA

ICC yathibitisha kupokea ombi la kutakiwa kuwachunguza viongozi wa Muungano wa NASA
by Sophia Chinyezi
Mahakama ya ICC Jumanne ilithibitisha kupokea ombi la kutakiwa kuwachunguza viongozi wa Muungano wa NASA. Wakenya wawili, kupitia kampuni ya uanasheria ya Canada, ilimwandikia barua Mkuu wa Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda kumtaka aanzishe uchunguzi dhidi Kinara wa NASA, Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka.
Kenneth Otieno na Martin Nkari wanaitaka mahakama hiyo kuwachunguza wawili hayo kwa madai ya uchochezi, na uhalifu mwingine ambao mahakama hiyo ina mamlaka ya kufuatilia.
Otieono ni Mwenyekiti wa Kundi la Sera za Kimataifa IPG, huku Nkari akiwa Katibu katika shirika hilo. Mkuu wa Kitengo cha Habari na Ushahidi, katika ofisi ya Bensouda, Mark Dillon amethibitisha kupokea stakabadhi za ombi hilo.?

Related Topics