Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Smart Minds Choose Us
★★★★ - on Play Store
Download App

Polisi wapata bunduki Saba nyumbani kwa Wanjigi huku wakizuiwa kumtia mbaroni

Polisi wapata bunduki Saba nyumbani kwa Wanjigi huku wakizuiwa kumtia mbaroni
By Suleiman Yeri
Maafisa wa polisi Jumanne, walifanikiwa kupata bunduki saba katika nyumba ya Mfanyabiashara Jimmy Wanjigi mtaani Muthaiga hapa jiji ambazo anadai analeseni za kuzimiliki. Bunduki hizo zimepatikana huku mahakama ikiagiza kutotiwa mbaroni kwake na kumpa dhamana ya shilingi elfu hamsini pesa taslimu.
Katika agizo lake Jaji Chacha Mwita ameamrisha Wanjigi asinyanyaswe hadi siku ya Alhamisi ambapo kesi aliyowasilisha na kutajwa kuwa yadharura itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Katika hati kiapo zake mbele ya Mahkama hiyo Mfanyabishara huyo amekana kufahamu shehena ya bunduki iliyopatika katika makazi yeke eneo la Malindi akisema si zake.
Aidha ombi hilo liliowasilishwa na Kampuni ya Uanasheria ya Murumba na Awele, Wanjigi anasema madai ya polisi kuwa anahusika na ulanguzi wa silaha haramu nchini ni njama ya kisiasa inayomharibia sifa.
Polisi vilevile wamezuiliwa dhidi ya kuharibu au kuvunja mali kiviyote vile hata hivyo hawakuzuiliwa kufanya masako katika biasahra zake na mali zake.
maafisa wa usalama wamekuwa wakiendeleza  msako katika nyumba zake kwenye Mtaa wa Muthaiga, Kwacha House mtaani Westlands na Caramel ABC Place hapa jijini.

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Fact-first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Follow The Standard on Google News

Related Topics