CORD yatoa makataa hadi Desemba 23, kwa makamishna wa IEBC kuondoka

Na Carren Omae

Ikiwa imesalia takribani miezi minane kabla ya uchaguzi mkuu ujao kuandaliwa, Muungano wa CORD umetoa makataa ya hadi Desemba 23 kuhakikisha wakamishana wapya wanateuliwa kuyatekeleza majukumu yao. Wakiwahutubia wanahabari mapema leo, Vinara wa muungano huo Raila Odinga na Kalonzo Musyoka, wamewataka makamishna wa sasa wakiongozwa na Isaac Hassan kukoma kuendeleza shughuli za IEBC wakisema kuwa wako ofisini kinyume cha sheria.
Kulingana na CORD, hatua hiyo ni njama ya kuipendelea Jubilee katika uchaguzi mkuu ujao.
Raila amedai kwamba IEBC imekuwa ikiendesha shughuli ya ukaguzi wa sajili ya wapiga kura kisiri.
Amesema Upinzani katu hautakubali kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu ujao, bila sajili mpya, na kwamba hautakubali kuendeshwa na maafisa wa sasa wa IEBC.
Aidha, vinara hao wa wanataka IEBC isitishe shughuli ya kutoa kandarasi hadi pale makamishna wapya watakapoingia afisini.