Serikali imesisitiza kwamba haitaruhusu adhabu ya vibiko dhidi ya wanafunzi katika shule za humu nchini. Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema haifai walimu kuwashurutisha wanafunzi kupata alama za juu katika mitihani.
Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Wagwer Kaunti ya Siaya, Waziri Magoha amesema mwalimu anayesemekana kumwadhibu kwa kumchapa mwanafunzi katika Shule ya Msingi ya Nyamninia atachukuliwa hatua. Magoha amesema maafisa wa polisi na wale wa Tume ya Huduma za Walimu TSC wanashirikiana katika uchunguzi huo.
Mwalimu huyo alikamatwa jana na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu.