Matiang'i atoa hakikisho la usalama

Na, Rosa Agutu
Matiang'i atoa hakikisho la usalama
Kaimu Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi Fred Matiang'i amesema usalama umedumishwa maeneo yanayo aminika yanaweza kuwa na vurugu, na maeneo ambayo hivi majuzi yamevamiwa na washukiwa wa kundi la kigaidi la Al shabaab.
Akizungumza katika kikao kilicho andaliwa na Baraza la Kitaifa la Makanisa NCCK kilichohusisha Tume ya IEBC na wazee wanaowakilisha jamii mbali mbali nchini kuzungumzia matayarisho ya uchaguzi, Matiang'i amesema serikali imeleta ndege 4 aina ya M17 na magari yatakayo wezesha maafisa wa usalama kuzuru maeneo kwa urahisi, na piki piki elfu tatu zitakazo wasafirisha machifu.
Kamishina wa Tume ya IEBC Paul Kurgat amesema maafisa wa usalama 180,000 wametengwa kudumisha usalama na kutakuwa na maafisa wawili katika kila kituo.Kutakuwa na  waangalizi wa uchaguzi walioidhinishwa na Tume hiyo, kutoka Marekani, Uropa , nchini Kenya na bara Afrika Kwa jumla. Miongoni mwao ni John Kerry wa Marekani
Akizungumzia suala la wapiga kura 5000 ambao alama za vidole hazionekani katika mashine, kama wanaofanya kazi ya ujenzi na wanao vuna kahawa, Kurgat amesema wapiga kura hao wanashauriwa kubeba vitambulisho vitakavyo kaguliwa na mashine maalum. Wapiga kura watakao subiri matangazo, watasimama mita 400 kutoka kituo cha kupiga kura.
Inspekta Mkuu wa Polisi,  Joseph Boinnet amesema usalama utadumishwa wakizangitia haki za kibinadamu, vilevile watashirikiana na idara zote za usalama kudumisha usalama msimu huu wa uchaguzi.

Related Topics