Serikali yasema baa la njaa limethibitishwa

Na Rosa Agutu/Beatrice Maganga

Huku kaunti mbalimbali zikiendelea kuathiriwa na ukame, Msemaji wa Serikali, Eric Kiraithe amesema serikali imeweka mikakati kuwasaidia waathiriwa.  Kiraithe amesema tayari shilingi milioni 250 zimetengwa kuwanusuru walioathirika huku serikali kuu ikiendelea kushirikiana na zile za kaunti kutafuta suluhu ya kudumu.

Kiraithe aidha ametoa wito kwa serikali za kaunti kuwahimiza wakulima kutenga sehemu za kupanda nyasi ili kupunguza vifo vya mifugo wakati wa ukame.

Kwenye kikao tofauti mapema leo, Waziri wa Kilimo Willy Bett alisema licha ya kiangazi kinachoshuhudiwa kwenye kaunti ishirini na tatu kote nchini, serikali ina chakula cha kutosha kuwalisha wananchi.

Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni kaunti za Taita Taveta, Kilifi na Kwale na maeneo ya Mashariki ya Nchi.