Mechi mbili za ligi ya soka nchini kufanyika jioni ya leo

Na,Hassan Ali

 Jioni ya leo kumeratibiwa mechi mbili za ligi ya soka nchini. Mjini Nakuru uwanjani Afraha itakuwa zamu ya wenyeji Ulinzi Fc baada ya kulitwaa taji la vikosi vya majeshi Afrika Mashariki kuwalaki Posta Rangers waliowafunga Sofapaka bao moja kavu mnamo Jumapili. Mjini Thika vijana wa James Nandwa wanawasubiri vijana wa Bandari ambao watakuwa wakijitupa ugani wakiwa na mwaki kufuatia ushindi wao wa taji la KECOMO mjini Nakuru wikiendi iliyopita.