Makamishna wa EACC waonywa dhidi ya kutoa taarifa kuhusu madai ya ufisadi yanayomkabili mwenyekiti wao

Na, Carren Omae

Makamishna wa EACC waonywa dhidi ya kutoa taarifa kuhusu madai ya ufisadi yanayomkabili mwenyekiti wao

Siku moja tu baada ya Makamishna  wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC kumtaka mwenyekiti wake Philip Kinisu kujiuzulu ili kutoa nafasi ya uchunguzi dhidi yake kufanywa, Mahakama ya Juu imetoa agizo la kuwazuia makamishMA  wa Tume hiyo kutoa taarifa zozote kufuatia uchunguzi uneoendelea kuhusu kampuni inayohusishwa na Philip Kinisu.
Kwenye uamuzi wake Jaji Edward Muriithi amewazuia Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC Halakhe Waqo, Naibu wake Michael Mubea Makamishna  Sophia Lepuchirit, Dabar Maalim, Paul Gachoka na Rose Macharia kuzungumzia suala hilo.
Ni jana ambapo makamishna hao walisema kwamba wamemwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali Professa Githu Muigai wakitaka ushauri zaidi. Walisema kuhusishwa kwa Kinisu na kampuni ya Esaki Limited huenda kukahujumu uchunguzi ambao umekuwa ukiendelezwa na tume hiyo dhidi ya kampuni zinazofanya biashara na NYS.
Ikumbukwe kampuni kadhaa zilizofanya biashara na taasisi hiyo zimeshtumiwa kwa kunufaika na shilingi takriban milioni mia saba zilizofujwa kupitia taasisi hiyo. Kinisu ameapa kutojiuzulu hadi atakapobainishiwa makosa yake.