Miili ya Watu Watatu Inayoaminika kuwa ya Wakili Willie Kimani, Mteja Wake na Dereva wa Texi Yapatikana

 

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, MIILI ya watu watatu inayoaminika kuwa ya Wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa Texi walioripotiwa kutoweka siku kadhaa zilizoipta, imepatikana kando ya mto Oldonyo Sabuk eneo la Kilimambogo.

Polisi wamesema kuwa miili hiyo imepatikana mapema leo huku taarifa za hivi punde zikiarifu kuwa mwili wa wakili huyo umetumbukia kwenye mto huo wakati wa shughuli ya kuiondoa iliko patikana.

Kufutia shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu kuhusu kisa hicho, Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinett sasa anataka maafisa watatu wanaohusishwa na kisa hicho wachukuliwe hatua za kisheria.

Wakili Kimani alitoweka na mteja wake Josphat Mwenda ambaye aliwasilisha kesi mahakani dhidi ya  afisa mmoja kwa kumpiga risasi.

Aidha, wawili hao na dereva wa texi waliloabiri walitoweka baada ya kuondoka katika mahakama ya Mavoko.

Related Topics

willie kimani