Michuki: Nitamshtaki Muite 9/04/09

Waziri wa mazingira wa Kenya John Michuki amemkashifu na kuchukua hatua ya kumfikisha mahakamani mbunge wa zamani wa Kabete Paul Muite kwa madai ya kumchafulia jina. Hapo Jumatano Muite alidai kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya kuarifiwa kwamba kikosi maalum cha polisi kiliagizwa kumuua. Alisema kikosi hicho kilianza kumchunguza baada yake kukemea vikali mauaji ya kiholela, kufuatia kuuwawa kwa watetezi wa haki wa shirika la Oscar.