Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Kenya’s Boldest Voice
★★★★ - on Play Store
Download App

Serikali yaonya watakaokaidi

Na, Beatice Maganga/  Mate Tongola
Serikali yaonya watakaokaidi
Serikali imetangaza siku ya Jumanne wiki ijayo kuwa likizo, kwa ajili ya hafla ya kuapishwa kwa Rais Mteule, Uhuru Kenyatta. Serikali aidha imeuonya Muungano wa NASA dhidi ya kuandaa halfa zozote au shughuli ambazo zitakuwa kinyume na sheria ikizingatiwa kwamba umetishia kumwapisha kinara wake, Raila Odinga sambamba na shughuli ya kumwapisha Kenyatta.
Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, Msemaji wa Serikali, Eric Kiraithe amesema mikutano yoyote ya kisiasa haitaruhusiwa bila kibali cha idara ya polisi pamoja na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Kiraithe ameitaja mipango ya NASA ya kumwapisha Raila sambamba na hafla ya kumwapisha Rais Kenyatta kuwa inayokiuka sheria.
Aidha, Kiraithe amesema serikali itawaadhibu wawakilishi wadi wanaoshiriki vikao katika mabunge ya kaunti kujadili na kupitisha kubuniwa kwa mabunge ya wananchi, akiitaja hatua hiyo kuwa inayokiuka katiba. Waandamanaji wanaopora mali ya umma kutekeleza uharibifu vilevile wameonywa vikali.
Hayo yanajiri huku Kaimu Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i akitangaza Novemba 28 kuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya kumwapisha Rais Kenyatta. Wakati uo huo kamati-andalizi ya halfa hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Joseph Kinyua imeuchapisha Uwanja wa Kasarani kuwa utakaotumika kwa shughuli hiyo iliyoratibiwa kuanza saa nne asubuhi siku ya Jumanne.
Kulingana na sheria, siku ya kumwapisha Rais hustahili kufanywa likizo, vilevile kuchapishwa kwa eneo la kufanyia sherehe hiyo katika gazeti rasmi la serikali. Naibu wa Rais, William Ruto vilevile ataapishwa huku Msajili wa Mahakama, Anne Amadi akiongoza shughuli hiyo mbele ya Jaji Mkuu, David Maraga. Viongozi wa mataifa zaidi ya ishirini wanatarajiwa kuhudhuria huku serikali ikutuma barua za mialiko kwa viongozi mbalimbali, akiwamo aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama na Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Fact-first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Related Topics