×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Uchunguzi wa kifo cha mwanahabari wa Pakistan waendelea

News

Upasuaji wa mwili wa mwanahabari raia wa Pakistani, Arshad Sharrif aliyeuliwa  nchini Kenya umefanywa kubainisha jinsi alivyoaga dunia.

Mwanahabari huyo anasemekana kuuliwa kimakosa na maafisa wa polisi katika barabara ya Magadi- Kajiado akidhaniwa kuwa mshukiwa wa uhalifu aliyekuwa akisakwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, maafisa wa trafiki walikuwa wameagizwa kusimamisha gari linalofanana na alilokuwa ndani na ambalo lilikuwa likiendeshwa na kakaye Kumran Khan. Khan hata hivyo aliponea akiwa na majeraha huku Arshad akiaga dunia papo hapo, polisi wakisema wawili hao walikataa kusimama walipoashiriwa kufanya hivyo na polisi.

Maujia ya mwanahabari huyo aliyekuwa na umri wa miaka hamsini yameshtumiwa vikali na wanahabari wa humu nchini na hata kimataifa.

Tayari mamlaka ya kutathimini utendakazi wa Maafisa wa Polisi IPOA imeanza uchunguzi kufuatia kuuliwa kwa mwanahabari huyo.

Arshad ametajwa kuwa mwanahabari mpekuzi mtajika nchini Pakitsan na alikuwa ametoroka taifa hilo kuepuka kukamatwa kufuatia makala ya upekuzi kwa jina 'Behind Closed Doors' aliyokuwa akifanya kuhusu utakatishaji wa fedha unaohusu watu wenye mamlaka makuu nchini humo.

Mwili wake umepatikana katika Hifadhi ya Maiti ya Chiromo ukiwa na alama mbili za kupigwa risasi.

Haya yanajiri huku mwanahabari mpekuzi, John Allan Namu akipinga kwenye Twitter madai kuwa alikuwa akishirikiana na marehemu kufanya taarifa moja ya upekuzi.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles