×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Tuju avunja kimya chake kuhusu madai ya Chebukati

Living

Mkurugenzi Mkuu Chama cha Azimio la Umoja One Kenya Raphael Tuju amevunja kimya chake kuhusu madai yaliyoibuliwa katika hati kiapo ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Wafula Chebukati kwenye rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

Katika kikao na wanabari, Tuju ambaye amekiri kukutana na Chebukati amejitetea akisema walikutana naye akiwa na watu wengine na hivyo madai ya kuwa alilenga kushawishi matokeo ya uchaguzi ni uongo.

Tuju ambaye anasema alijaribu zaidi ya mara tatu kumwona Chebukati, alifanya hivyo baada ya kufahamishwa kuhusu kufutwa kwa fomu za 34A kwenye mtandao wa IEBC na kutundikwa kwa fomu nyingine katika wavuti huo, madai ambayo Tuju anasema aliyawasilisha kwa Idara ya Upelezi DCI. Aidha Tuju anasema jamaa aliyemfahamaisha alikuwa mfanyakazi wa IEBC ambaye alitishiwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC Marjan Hussein Marjan, alipojaribu kumfahamisha kuhusu kubadilishwa kwa fomu hizo.

Tuju ambaye anasema alilazimika kuingia ofisini kwa Chebukati kutaka kujua kuhusu kilichokuwa kikiendelea, aidha anaongeza kwamba, alizuiwa langoni na walinzi wa Chebukati hali ambayo ilisababisha kuingia kwa nguvu ili kumfahamisha kilichokuwa kikiendelea.

Vilevile Tuju amedai kwamba baada ya kufanikiwa kuingia ofisini kwa Chebukati na kuanza mazungumzo kuhusu kubadilishwa kwa fomu za 34A, alimpata akiwa na Profesa Abdi Guliye na Kamhna Boya Molu, ambapo baada ya muda mchache, Guliye aliomba radhi na kwenda msalani akiwa na simu yake na kuchukua muda mrefu. Aidha ameongeza kwamba mlangoni palikuwa na viongozi wa UDA ambao walikuwa wakisubiri kuingia ofisini humo.

Aidha Tuju amemtaka Chebukati, Profesa Abdi Guliye vilevile Kamishna Boya Molu kuweka wazi kuhusu ziara yao nyumbani kwake katika eneo la Karen. Tuju ametishia kuweka wazi video za kamera za CCTV zilizowanasa nyumbani kwake pamoja na mazungumzo waliyokuwa nayo.

Wakati uo huo Tuju amedai kwamba Guliye aliwatuma watu wawili nyumbani kwake, ambao hakutaka kuwaweka wazi kwa vile ni mashahidi katika rufaa iliyowasilishwa kwenye Mahakama ya Juu.

Katika hati kiapo yake, Chebkati alidai kwamba Naibu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Luteni Francis Ogolla, Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai, Wakili wa Serikali Kennedy Ogeto na Katibu Mkuu wa Wizara Ofisi ya Rais Kennedy Kihara kuwa miongoni mwa maafisa wakuu wa serikali waliomshinikiza kuyakarabati matokeo ya uchaguzi wa urais ili Raila awe mshindi ama kuwapo na marudio ya uchaguzi wa urais. Kulingana naye, maafisa hao walidai kwamba hali hiyo itahakikisha amani inadumishwa nchini.

Aidha Chebukati anadai kwamba Naibu wake Juliana Cherera, Makamishna Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang'anya kuwa walioitikia mashinikizo hayo.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles