Abraham Serem ndiye Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya KenGen baada ya kuteuliwa kushikilia wadhifa huo. Serem anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Rebecca Miano ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Maeneo Kame na Maendeleo katika Maeneo. Katika notisi iliyochapishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kengen, Samson Mwathethe kwenye magazeti ya humu nchini leo hii, imesema kwamba Serem atahudumu katika wadhifa huo hadi wakati mtu mwingine atakapoteuliwa kwa wadhifa huo. Serem amekuwa akihudumu katika wadhifa wa Meneja Mkuu vilevile mkuu wa wafanyakazi tangu Machi mwaka 2016. Ana tajriba ya miaka 20 katika kitengo cha kuwahudumia wafanyakazi, HR.
Facts First
This story continues on The Standard INSiDER. Subscribe now for unfiltered journalism that holds power to account.
Already have an account? Login
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.