×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Rais William Ruto aongoza kuapishwa kwa majaji sita walioachwa nje na Uhuru

Living

Rais William Ruto ametimiza ahadi yake ya kuwaapisha majaji sita walioachwa nje wakati wengine arobaini walipoapishwa na Rais Mstaafu, Uhuru Kenyatta. Akizungumza wakati wa halfa hiyo katika Ikulu ya Nairobi ambayo pia imehudhuria na aliyekuwa Jaji Mkuu, David Maraga wakati uteuzi wa majaji hao ulipokataliwa na Uhuru, Rais Ruto amesisitiza umuhimu wa kuiheshimu Idara ya Mahakama na idara nyingine huru na kuzipa nafasi ya kutekeleza majukumu yao bila mwingilio.

Ruto ametoa changamoto kwa Idara ya Mahakama kuzishughulikia kwa wakati hasa kesi za ufisadi ambazo anasema zimekuwa zikichukua muda mrefu mahakamani.

Mmoja baada ya mwingine waliokuwa majaji wa Mahakama Kuu, Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir Profesa Joel Ngugi wameapishwa kuhudumu katika Mahakama ya Rufaa.

Aidha Evans Makori na Judith Omange wameapishwa kuhudumu katika Mahakama ya Mazingira na Ardhi.

Akizungumza baada ya kuwaapisha siku moja tu baada ya kuahidi kufanya hivyo, Rais Ruto amewapongeza majaji hao huku akizungumzia namna walivyolazimika kusubiri kwa muda mrefu baada ya kukosa kuapishwa.

Ikumbukwe Rais Mstaafu, Uhuru Kenyatta alikataa kuwaapisha akidai kwamba Ripoti ya Idara ya Ujasusi, NIS ilitilia shaka maadili yao.

Ruto ameelezea haja ya kuiunga mkono Idara ya Mahakama katika utekelezaji wa majukumu yake huku akiahidi kutokuwa kizingiti kwa idara hiyo na kwamba atakuwa tayari kushauriana nayo panapohitajika. Amesisitiza kwamba hakuna aliye juu ya sheria na ni lazima iheshimiwe na kila mtu bila kujali wadhifa wake.

Ruto aidha ametoa changamoto kwa idara hiyo kumakinika katika kuzishughulikia kesi za ufisadi na mizozo ya kibiashara ambazo mara nyingi huchukua muda mrefu mahakamani.

Jana aidha, Ruto aliahidi kuwa serikali yake itaiongezea idara ya mahakama bajeti ya shilingi bilioni 3 kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Halfa ya kuwaapisha majaji hao imeongozwa na Msajili wa Idara ta Mahakama, Ann Amani kwa usaidizi wa Mkuu wa Utumishi wa Umma, Joseph Kinyua. Wengine waliohudhuria halfa hiyo ni Naibu wa Rais, Rigathi Gachahua, Jaji Mkuu, Martha Koome na naibu wake Philomena Mwilu, aliyekuwa Jaji Mkuu, David Maraga, majaji wengine na familia za majaji walioapishwa.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles