Maafisa wa Kitengo cha Kukabili Ugaidi ATPU jijini Nairobi wanachunguza kisa ambapo bastola 22 na risasi 565 zimepatikana ndani ya nyumba moja katika Mtaa wa Wood Avenue, Kilimani.
Inaarifiwa kuwa polisi walipata sialaha hizp walipokuwa wameenda kushika doria wakati wa kutwaa mali baada ya mmliki wa nyumba hiyo kushindwa kulipa kodi ya shilingi milioni 4.9.
Polisi wanasema mwenye deni alikuwa amepata agizo la mahakama kutwaa mali, na walipovunja milango walipata chumba kimoja kilichokuwa hifadhi ya silaha.
Aidha, walipata stakabadhi za usajili wa silaha hizo.
Mkuu wa Polisi wa Kilimani, Stephen Sanki amesema uchunguzi tayari umeanziswa ili kubaini iwapo mshukiwa alikuwa mfanyabiashara wa silaha na endapo ana kibali cha kuzimiliki ama la.
Vilveile, polisi wanasema kuwa muda wa leseni ya mmiliki wa silaha hiyo aliyetambuliwa kwa jina Ken Lugwili uliisha mwaka 2018.
Polisi wamempa makataa ya saa ishirini na nne mshukiwa ambaye anasekemana ameenda mafichoni kujisalimisha.
Silaha hizo zinazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani.
Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria, raia wenye leseni ya kumiliki silaha wanastahili kukaguliwa kila mwaka.
Sheria hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2018 baada ya kuongezeka kwa leseni gushi zilizokuwa zikitumika nchini.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.