×
App Icon
The Standard e-Paper
Join Thousands of Readers
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Wabunge wapendekeza sheria ya kuthibiti hafla ya kuchangisha fedha "Harambee"

Living

Na, Carren Omae

Mjadala mkali umeibuka katika Bunge la Kitaifa kuhusu Mswada wa kudhibiti hafla za kuchangisha fedha maarufu, harambee. Mswada huo ulioasisiwa na Seneta wa Kisumu, Profesa Anyang' Nyong'o umewasilishwa bungeni na Kamati ya Haki na Sheria. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Samwel Chepkonga amesema mswada huo unalenga kuhakikisha uwajibikaji kwa fedha zinazochangishwa. Aidha anasema mswada huo utakabili tatizo la ufisadi miongoni mwa masuala mengine. Mbunge wa Kiminini, Chris Wamalwa ni miongoni mwa waliounga mkono mswada huo akisema baadhi ya wapigakura wamekuwa wakitumia hafla hizo kuwakandamiza wanasiasa hasa wakati wa uchaguzi. Hata hivyo wabunge wengi wameupinga mswada huo wakisema Wakenya wengi hasa kutoka jamii maskini ndio watakaoathirika. Mbunge wa Mbitha, Millie Odhiambo amepinga pendekezo kwenye mswada huo kwamba ni Kamati ya Kitaifa itakayosimamia hafla hizo ibuniwe. Aidha wapo waliopendekeza mswada huo kufanyiwa marekebisho kabla ya kupitishwa. Kubai Kiringo ni Mbunge wa Igembe ya Kati.  

 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles