Na, Mike Nyagwoka
Benki ya Cooperative imekuwa ya kwanza kutangaza viwango vipya vya riba kufuatia sheria mpya ya kudhibiti riba ya mikopo inayotolewa na benki. Afisa Mkuu Mtendaji wa benki hiyo, Gideon Muriuki amesema Cooperative haitawatoza wateja wake riba inayopita asilimia 14.5 kuanzia sasa. Haya yanajiri huku chama cha wahasibu, ICPAK kikiwashauri washikadau katika sekta nzima ya benki kufanya mabadiliko kuhusu viwango vya riba. Aidha chama hicho kupitia Mwenyekiti wake, Fernades Barasa kimeitaka serikali kuandaa sheria itakayodhibiti mashirika mengine ya kutoa mikopo kama vile vyama vya ushirika na watu binafsi kwa Kiingereza Shylocks.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.