Na,Sophia Chinyezi
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Keriako Tobiko amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuamwachilia kwa dhamana raia wa Uingereza aliyeshtakiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya. Tobiko anasema huenda Jack Marrian akakosa kuhudhuria vikao vya kesi dhidi yake. Mapema leo, Mahakama ya Kibera imemwachilia Jack kwa dhamana ya shilingi milioni sabini na wadhamini wawili, kwenye kesi ya ulanguzi wa dawa aina ya cocaine zenye thamani ya shilingi milioni 598. Dawa hizo zilipatikana kwenye Bandari ya Kilindini Mombasa. Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kibera, Derrick Kuto ameagiza Marrian awe akifika katika ofisi ya mpelelezi katika kesi hiyo mara moja kila wiki. Wakati uo huo Mkenya, Roy Francis Mwanthi, ambaye anakabiliwa na mashtaka sawa hayo, ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni sitini na wadhamini wawili. Hata hivyo upande wa mashtaka umeeleza kutoridhishwa na uamuzi wa kuwaachilia wawili hao kwa dhamana na kusema watakataa rufaa.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.