×
App Icon
The Standard e-Paper
Informed Minds Prefer The Standard
★★★★ - on Play Store
Download Now
×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Raila Asema Sheria za Matiang'i Zimefeli

Living

Na, Beatrice Maganga Sheria mpya za elimu zilizobuniwa na Waziri Fred Matiang'i zimefeli. Ndiyo kauli ya Kinara wa CORD Raila Odinga ambaye amesema huenda visa vya moto shuleni vinachochewa na sheria hizo. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari akiwa kwenye jimbo la Philadelphia Marekani, Raila  ameikosoa sheria kwamba wanafunzi wasio watahiniwa wasalie nyumbani wakati wa mitihani ya taifa, akisema hatua hiyo si suluhu ya udanganyifu kwenye mitihani hiyo. Aidha amekosoa hatua ya Matiang'i kupiga marufuku maombi muhula wa tatu na suala la wanafunzi kutembelewa na wazazi wao muhula huo. Ameitaka serikali kudhibiti udanyanyifu wa mitihani kuanzia Baraza la Mitihani nchini KNEC ambalo hutunga mithani hiyo badala ya kuwalazimishia wanafunzi sheria zisizo na msingi. Wakati uo huo ameitaka serikali kuwahakikisha wanafunzi usalama wao ikizingatiwa kwamba visa vya moto shuleni vinaendelea kuripotiwa kila kukicha.

 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Articles