Mahakama Kuu leo alasiri inatarajiwa kutoa sababu za kutoachiliwa kwa wabunge wanane wanaozuiliwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi.
Aidha, muungano wa CORD jana uliwasilisha kesi ya kutaka wabunge wake waachiliwe kwa dhmamana bila mafanikio.
Hadi sasa vinara wa CORD Raila Odinga, Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka pamoja na Gavana wa Nairobi Evans Kidero, ni miongoni mwa viongozi ambao wamewasili katika Kituo cha Polisi cha Pangani ambako baadhi ya viongozi wa muungano huo wanazuiliwa kwa siku ya pili sasa.
Miongoni mwa wanaozuiliwa ni Seneta wa Machakos Johnston Muthama, Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa, Wabunge Moses Kuria wa Gatundu Kusini, Junet Mohamed wa Suna Mashariki na Ferdinand Waititu wa Kabete.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.