Mkutano ulioibuka na hendisheki baina ya Jomo Kenyatta na Ronald Ngala mbele ya wakoloni Waingereza. [Pambazuko]
Kama kunalo fungu la watu ambao wamechezwa shere miaka mingi katika mipangilio ya mfumo unaoletwa na mapendekezo ya BBI, bila shaka ni Wakenya wanaoishi jimbo zima la pwani ya Kenya. Wameshuhudia BBI chungu nzima tangu jadi ya kuwakaribisha wageni wa mwanzo ambao hatimaye waliwageukia kuwafanya bidhaa za kuwauzia milki za kigeni, Ghuba la uajemi na Bara Ulaya.