Wanamuziki wa injili wakiwemo Ben C (kushoto) Dar Mjomba,Princess Farida and Warda wakiwa Groove Tour 2017 katika Machakos People's Park, Machakos. [Picha/Elvis Ogina ]
Wale ambao walikuwa wafuasi wa minenguo ya rhumba na chakacha katika miaka ya mwanzoni hadi miaka ya 1990s, bila shaka jina la Princess Farida kwao silo geni. Farida ambaye alililipata jina lake hili kwa ushindi wa miaka mfululizo katika mashindano ya mnenguaji wa dansi ya “Chakacha”, miaka ya tisini, amekuwepo ulingoni mwa muziki kwa zaizi ya miaka 20 na hivi ametoka jikoni na kibao kipya cha Ra? ki wa Kweli kinachofuatia kingine kinachoendelea kubobea cha Amelipa.