Wakati umewadia saratani kutangazwa janga la kitaifa

Nusura wa ugonjwa wa saratani John Kiptanui Rono akionyesha alama ya upasuaji. [Standard]

Ijumaa iliyopita, taifa liligubikwa na huzuni baada ya Mbunge wa Kibra Ken Odhiambo Okoth kuaga dunia kutokana na saratani ya utumbo.  Mbunge huyo mwenye umri wa 41 alikuwa ameugua ugonjwa huo kwa muda mrefu. Alisa? ri Paris, Ufaransa, kwa matibabu zaidi. Yapata siku tatu baadaye, taifa lilipokea tena habari za tanzia kwamba Gavana wa Kaunti ya Bomet, Joyce Laboso, ameaga dunia kutokana na saratani. Alikuwa na umri wa miaka 58.

Kabla ya kifo chake, mwendazake alikuwa nchini India baada ya kutoka Uiengereza ambako alikuwa akipata matibabu kwa muda kabla ya kurudi hospitali ya Nairobi. Mnamo mwezi Aprili mwaka huu, aliyekuwa mwendeshaji wa magari za mbio za Safari aliyekuwa pia mwanawe Rais Mstaafu Moi, Bwana Jonathan Toroitich, aliaga dunia baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu. Miaka mitano iliyopita, mchezaji mashuhuri wa kriketi nchini Emmy Jepng’etich Ruto maarufu kama Jepkriket bintiye aliyekuwa Gavana wa Bomet Bwana Isaac Ruto aliaga dunia mwaka 2014 kutokana na sarati ya damu. Orodha haikomei hapo. Wiki chache tu zilizopita, Mkurugenzi Mkuu Mtandaji wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom Bob Collymore, aliaga dunia nyumbani kwake akiwa anaendelea kupokea matibabu ya ugonjwa wa saratani.

 Mwanahabari wa NTV Janet Kanini aliaga dunia mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 38 kutokana na saratani. Naye aliyekuwa Gavana wa Nyeri Nderitu Gachagua aliaga dunia mwaka wa 2017 baada ya kupokea matibabu kwa muda wa miaka miwili kule London kutokana na saratani ya nyongo. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Wanawake nchini Bii Jane Kiano aliaga dunia mwaka wa 2018 akiwa na umri wa miaka 74 kutokana na saratani ya mapafu.

 Naye aliyekuwa Mbunge wa Baringo Kusini Bii Grace Kipchoim aliaga dunia Aprili mwaka uliopita kutokana na saratani ya utumbo. Ugojwa wa saratani umekuwa tishio kwa maisha ya Wakenya huku ikiwaathiri wakuu na wananchi wa kawaida kwa kiwango kinachokua kwa kasi sana ikilinganishwa na magojwa mengine yasiyo ya kuambukiza. Katika eneo la Africa Mashariki Kenya inaongoza kwa kuripoti idadi kubwa ya wanaoathirika kutokana na ugonjwa wa saratani ikilinganishwa na mataifa ya Uganda na Tanzania.

 Takwimu kutoka idara ya KEMRI zinaonyesha kuwa visa vipya vya ugonjwa wa saratani vime? kia zaidi ya 37,000 kila mwaka huku 80% ya visa hivi vikigunduliwa kwa kuchelewa. Hata hivyo, serikali imejibidiisha kuhakikisha kwamba janga la ugonjwa wa saratani linatokomezwa kabisa. Miongoni mwa mikakati yaliyowekwa na wadau katika sekta ya afya kuzuia Wakenya kwenda mataifa ya ugaibuni kupata matibabu ya saratani kwa kutumia miale ni pamoja na kubuniwa kwa kitengo cha kushughulikia waathiriwa wa ugonjwa wa saratani katika Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa Kenyatta, jijini Nairobi.

 Aidha, kumekuwa na wito kutoka kwa mashirika ya kiafya nchini wa kushinikiza serikali kutangaza ugonjwa wa saratani kuwa janga la kitaifa kama njia ya kuimarisha jitihada za kukabili ugonjwa huu na kuokoa fedha zinazotumiwa na waathiriwa wa janga hili kuzuru mataifa ya India, Uingereza, Ufaransa na Afrika Kusini, kutafta tiba ya ugonjwa huu.

Wataalam kwenye sekta ya afya wanahoji kuwa ugonjwa wa saratani unaweza kutibiwa endapo inabainika kupitia vipimo maalum, hivyo basi madaktari kuwashauri watu wote kukumbatia mpango wa kupimwa maambukizi ya ugonjwa wa saratani kila wanapotembelea kituo cha afya ili kubaini na kuanza kupokea matibabu haraka iwezekanavyo kinyume na ilivyo sasa ambapo wengi wa waathiriwa wanagunduliwa wikiwa katika hatua iliyopita matibabu.

Mapendekezo mengine kuhusu njia ya kukabiliana na janga la saratani ni kupitia kula vyakula asilia na kuepuka kwa vyovyote matumizi ya mihadarati na uvutaji wa sigara na bhangi. Uta? ti unaonyesha kuwa ulaji wa aina tano ya matunda kila siku inapunguza maradufu uwezekano wa kupatwa na saratani.

 Hata hivyo, vyakula vilivyohifadhiwa kutumia chemikali ni hatari mno kwa afya na kwa kiwango kikubwa kuwa miongoni mwa njia zinazochangia kuenea kwa saratani mwilini. Kulingana na uta? ti uliofanywa na shirika la Research 8020 na kufadhiliwa na Nairobi Hospice, kemikali za asbestos na a? otoxins kwenye vyakula zimechangia kwa kiwango kikubwa maambukizi ya ugonjwa wa saratani, ulaji wa vyakula bila mpangilio maalum wa kiafya umri na magonjwa kama vile maradhi ya ukimwi.