Wangwana wa kaunti ya Taita Taveta, nambari 006 kati ya kaunti 47 za Kenya wangali wamepigwa na butwaa wakati gavana wao Granton Samboja ambaye aliingia uongozini mwaka 2017 kwa tikiti ya kulazimishwa ya WIPER, alimkimbilia kiongozi wa upinzani Raila Odinga badala ya kinara wake wa chama Stephen Kalonzo Musyoka kwa ushauri wa dharura kuhusiana na kusambaratika kwa serikali yake kufuatia mjuvyo wa kiutawala baina yake na wawakilishi (MCAs) wa wadi za Taita Taveta.
Habari za kuaminika zatujia kinaga ubaga kwamba Gavana Samboja huenda akahamia rasmi kwa chama cha ODM siku chache zijazo kubwaga chama cha WIPER, tayari kwa vita vyovyote vile vya siasa ya uchaguzi mpya mdogo wa kaunti endapo pendekezo lake la kuitaka serikali ya kaunti ya Taita Taveta ivunjiliwe mbali litatimia.