Asilimia 55 ya watoto hudhulumiwa kingono na maafisa wa polisi.

Ripoti ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu, KNCHR ikionesha kwamba asilimia 55 ya watoto hudhulumiwa kingono na maafisa wa polisi na asilimia 45 wakidhulumiwa na wananchi, Naibu Kamishna kwenye Kaunti ya Trans Nzoia,  Beatrice Bikeyo amewasihi Wakenya kutosalia kimya na kuwaripoti watu wanaodhulumu  watoto.

Mkurugenzi wa masuala ya watoto kwenye kaunti hiyo,  Pauline Mukasa ameutaja umaskini na utamaduni chanzo cha ongezeko la visa hivyo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa KNCHR, Daktari Benard Mugesa  amependekeza kufanywa kwa uhamasisho kwa umma kupitia mradi uitwao Imarisha Haki kufuatia ripoti hiyo

Related Topics

KNHCR