Bunduki zaibwa katika Kituo cha Polisi cha Kobuchoi, Nandi wakati maafisa walipokwenda kutazama mechi

Polisi wanaendeleza msako wa kurejesha bunduki tatu aina ya G3 ambazo ziliibiwa kutoka Kituo cha Polisi cha Kobujoi kwenye Kaunti ya Nandi.

Inaarifiwa kwamba washukiwa wa uhalifu waliingia kwenye chumba maalum cha kuhifadhi silaha na kuiba bunduki hivyo pamoja na risasi zaidi ya ishirini na kisha kutoweka nazo.

Kisa hicho kilitokea wakati maafisa wote kituoni humo walipokuwa wameenda kutizama mchuano kati ya Manchester United na Barcelona usiku wa kuamkia leo.

Kwasasa polisi zaidi wametumwa eneo hilo kuzisaka bunduki hizo.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

bunduki