Wakazi wa Eneo la Mamboleo kwenye Kaunti ya Kisumu wamemiminika kwenye Barabara ya Kisumu-Kakamega kujichotea sukari iliyomwagiga

Wakazi wa Eneo la Mamboleo kwenye Kaunti ya Kisumu wamemiminika kwenye Barabara ya Kisumu-Kakamega kujichotea sukari iliyomwagiga  baada ya lori lililokuwa limebeba bidhaa hiyo kupoteza mwelekeo na kubingiria huku dereva na taniboi wake wakipata majeraha.  Licha ya wakazi kupata riziki wasiokuwa wameitarajia, wametoa wito kwa mamlaka inayohusika kuikarabati sehemu ya barabara hiyo kwa kuweka matuta kwani ni takriban wiki moja tu ambapo ajali nyingine ilitokea kwenye eneo hilo.

Meneja wa mauzo wa duka la jumla ambalo lori yao limehusika kwenye ajali hiuyo, Hadson Muhatia, amesema waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga, Jijini Kisumu.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

road accidentspeeding lorry