Serikali imetenga kima cha shilingi bilioni 3 zitakazotumiwa kuboresha kilimo cha kahawa

Serikali imetenga kima cha shilingi bilioni 3 zitakazotumiwa kuboresha kilimo cha kahawa nchini. Akihutubu wakati wa Kongomano la Kimataifa la Kahawa linaloendelea katika Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta amesema mpango huo utaimarisha pakubwa ukuzaji wa zao hilo ambao umedidimia kwa muda.

Rais aidha amekitaja kilimo cha kahawa kuwa tengemeo kuu kwa familia nyingi hivyo kuwapo kwa haja ya kukiboresha.

Akihutubu wakati wa kongamano hilo, Waziri wa Kilimo, Mwangi Kiunjuri aidha amewashukuru wawekezaji kwa kuchangia ukuzaji wa sekta ya kahawa nchini, akisema juhudi hizo zitasaidia kuboresha mapato ya wakulima.

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.